TAARIFA YA KUZAMA KWA MELI IKITOKEA DAR ES SALAAM KWENDA ZANZIBAR
Meli iliyokuwa imewabeba takriban watu miambili
imethibitiswha kuzama katika bahari ya hindi eneo la Chumbe kisiwani
Zanzibar. Meli hiyo kwa jina Star Gate ilikuwa inatoka Dar Es Salam
kuelekea Zanzibar.
Kulingana na taarifa za vikosi vya wanamaji , meli hilyo ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali.Jeshi la polisi la wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo la Chumbeambalo ni umbali wa kilometa 13.8 kutoka bandari ya Zanzibar pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment