YALIYOMSIBU DR.STEVEN ULIMBOKA
Kamanda wa
polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na
waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata
kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano
wakati akipata kinywaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova
amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake
kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka
katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo
polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema
jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na
upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke
nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo
wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha
matukio mengine kama hayo
MENGINE
Akisimulia
mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt
Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha
tukio hilo.
Alisema alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.
Alisema alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.
Gari iliyokuwa imembeba Dr.Steven Ulimbika ikisukumwa na Wauguzi na Madaktari Hospitalini Muimbili