Thursday, June 28, 2012

YALIYOMSIBU DR.STEVEN ULIMBOKA

YALIYOMSIBU  DR.STEVEN ULIMBOKA

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinywaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
MENGINE 
 Akisimulia mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha tukio hilo.




Alisema alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.


Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.

 
Gari iliyokuwa imembeba Dr.Steven Ulimbika ikisukumwa na Wauguzi na Madaktari Hospitalini Muimbili

No comments:

Post a Comment